Simamia Logo

Simamia App

Usimamizi wa Kisasa
Sera ya Faragha

Tunajali Faragha Yako

Fahamu jinsi tunavyolinda na kusimamia data za biashara yako.

Simamia App imejitolea kulinda taarifa zako za biashara, mauzo, bidhaa, pamoja na taarifa za wateja wako kwa usalama wa hali ya juu.
Imeboreshwa Mwisho: 20 Julai 2026

0. Watu Wanaolengwa

Simamia App imeundwa kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) nchini Tanzania — hasa wanaoendesha maduka ya rejareja, migahawa, saluni, warsha, na biashara nyinginezo zinazohitaji usimamizi rahisi wa bidhaa, mauzo, madeni na taarifa za wateja.

App inapatikana kwa kila mtu mwenye umri wa miaka 13 na kuendelea ambaye anataka kurahisisha shughuli zake za biashara kwa njia ya kidijitali. Hakuna ubaguzi wowote kwa msingi wa jinsia, dini, au eneo la kijiografia ndani ya Tanzania.


1. Taarifa Tunazokusanya

Ili kukupatia huduma bora kupitia Simamia App, tunakusanya taarifa zifuatazo kulingana na njia uliyochagua wakati wa kuanza:

Njia za Kufungua Akaunti:

  • Kupitia Google: Tunakusanya barua pepe (email), jina, na picha ya wasifu kutoka kwa akaunti yako ya Google uliyotumia kuingia.
  • Kupitia OTP (Namba ya Simu au Barua Pepe):Tunakusanya namba ya simu au barua pepe uliyotumia kupokea namba ya uthibitisho (OTP) ili kuhakiki utambulisho wako.
  • Baada ya Uthibitisho: Ili kuunda au kujiunga na akaunti, tunakusanya jina la biashara yako na namba ya simu ya biashara.

Mtumiaji wa akaunti anapata majaribio ya siku 14 bila malipo (trial).

Kwa wenye akaunti, tunakusanya data zifuatazo unapoanza kutumia app:

  • Data za Biashara: Bidhaa, stock, mauzo, matumizi (expenses), faida, madeni, na oda.
  • Taarifa za Wateja: Namba za simu au taarifa unazoingiza kwa ajili ya oda, WhatsApp, au SMS.
  • Taarifa za Matumizi: Vipimo vya utendaji wa app, mipangilio yako, na data za kukusaidia kurejesha shughuli zako.

2. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

Taarifa zako hutumika kwa madhumuni yafuatayo pekee:

  • Kukuhakiki (verify) utambulisho wako unapojiandikisha au kuingia kwa njia ya OTP au Google.
  • Kufuatilia mwenendo wa biashara yako kupitia ripoti, historia ya mauzo, na faida.
  • Kusindika oda, kubadili hali ya malipo, na kurahisisha mawasiliano na wateja.
  • Kuhakiki malipo ya vifurushi kupitia Transaction ID.
  • Kukupa uwezo wa kurejesha data zako baada ya kufuta na kusakinisha upya app kupitia kuingia tena kwenye akaunti yako.
  • Kuboresha utendaji wa app na kuhifadhi mipangilio yako ya mwisho.

3. Uhifadhi na Ulinzi wa Data

Tunachukua hatua mbalimbali kuhakikisha data zako zinalindwa kwa usalama mkubwa.

Kwa Wenye Akaunti: Data zako huhifadhiwa kwenye seva zetu zilizolindwa kwa usimbaji fiche (encryption) na zinaweza kurejeshwa kwa kuingia tena kwenye akaunti yako.

Udhibiti wa Data:Unaweza kufanya Export DB au Import DB kupitia sehemu ya Settings ili kulinda taarifa zako. Kwa usalama zaidi, Export DB inahitaji namba ya siri (encryption ya tarakimu 4–6).

Kufuta Data:Ukichagua "Futa Data Zote", taarifa zako zote zitafutwa kabisa na hatua hiyo haiwezi kurejeshwa.


4. Ruhusa za Kifaa

Simamia App inaweza kuomba ruhusa zifuatazo ili vipengele vya mfumo vifanye kazi vizuri:

  • Kamera/Scanner: Kukagua barcode na QR code za bidhaa wakati wa kuongeza stock au kutafuta bidhaa.
  • Storage: Kupakua PDF, CSV, na kufanya bulk import ya bidhaa.
  • Simu & Mawasiliano: Kupiga simu au kutuma WhatsApp/SMS moja kwa moja kwa wateja wako.

5. Mabadiliko ya Sera Hii

Tunaweza kuboresha sera hii mara kwa mara ili kuendana na mabadiliko ya sheria au maboresho ya vipengele vipya vya Simamia App. Mabadiliko yoyote yatajulishwa ndani ya app na tarehe ya "Imeboreshwa Mwisho" itasasishwa.


6. Wasiliana Nasi

Kama una maswali, maoni, au unahitaji msaada kuhusu sera hii ya faragha, unaweza kuwasiliana nasi kupitia:

Simu: +255 798 700 900

Msaada: Angalia video za mwongozo ndani ya app au tembelea ukurasa wetu wa Help Center.

Chat with us